Skip to main content

VYAKULA MUHIMU ZAIDI KWA MAMA MJAMZITO

LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NI MUHIMU SANA, KWANI LISHE HII HUTUMIKA KWA MAMA NA MTOTO ANAENDELEA KUKUA TUMBONI. KWA KAWAIDA MAHITAJI YA CHAKULA NA VIRUTUBISHO MWILINI MWA MWANAMKE HUONGEZEKA WAKATI WA UJAUZITO NA KADRI UJAUZITO UNAVYOENDELEA KUKUA, VIRUTUBISHO HIVYO HUTUMIKA KUJENGA MWILI WA MAMA NA MTOTO. HIVYO MAAMUZI YA LISHE AU LISHE MAMA ANAYOPATA HUATHIRI PIA MAENDELEO YA MTOTO ANAYEKUA MWILINI MWAKE. TUTAONA VYAKULA MUHIMU VYA KUZINGATIA LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NA BAADHI YA VITU VYA KUKWEPA.
Related image
Mama mjazito akipata mlo wenye mboga za majani
Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini;

Nafaka na Vyakula vya Wanga.
Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka mbalimbali(mahindi,mtama,ulezi n.k), viazi, ndizi, mihogo. Ni vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili(whole grains) kama mahindi, ngano na mchele usiokobolewa; cereals n.k.cereals

Nyama, Samaki na Vyakula vya Protini.
Hivi ni muhimu kwenye kuujenga mwili, hasa kipindi cha miwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya mtoto vinajengwa. Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri. Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi, senene, panzi na wanyama wengine ; vyanzo vya protini za mimea kama maharage, soya, njugu, njegere, karanga,korosho n.k . Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo vingine vya protini muhimu.vaykula vya protini maziwa

Vyakula vya Mafuta.
Hutumika kwenye kuupatia mwili nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili. Mara nyingi vyakula kama nyama, karanga, ufuta, alizeti,senene, panzi, samaki na matunnda kama maparachichi huwa na mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza mafuta yenye lehemu(cholesterol) nyingi.

Mboga za Majani na Matunda.
Matunda na mboga za majani ni sehemu muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula. Vitamini husaidia kuimarisha kinga ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili. Madini kama ya chuma, kalsiamu, zinki, madini joto(Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto tumboni mwa mama.mboga za majani Vitamini B9 (Foliki asidi) na madini ya chuma hutolewa kama virutubisho ziada kliniki wakati wa ujauzito ili kutosheleza mahitaji ya mwili na kuzuia hatari ya upungufu wa damu kutokea.matunda

Maji
Maji ni muhimu kwenye mmenyenyo na unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya lita 2.3 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, soda, au maji yenyewe. Ni vema zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda.

Mfano wa Mpangilio wa Mlo.
Ili kuhakikisha mlo kamili mjamzito anaweza kufuata mfano wa mpangilio wa mlo ufuatao;

Mfano,
Mlo wa Asubuhi: A - Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi, B - Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua,Uji C - Karoti D - Mayai, E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya
Mlo wa Mchana: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa, B - Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi C - Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya.
Mlo wa Usiku: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa, B - Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati C - Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya Soya.
Vitu na Vyakula vya kuepuka/kupunguza
Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto. Haishauriwi kutumia pombe kabisa!
Uvutaji Sigara
Kupunguza unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.
Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi amabayo ni mbaya kwa afya.

Comments

  1. Nashukuru kwa kutufahamisha kumbe sijatoka sana nje na mpangilio wa chakula nnavomuhudumia mkewangu mjamzito

    ReplyDelete
  2. Asantee saana nawafatilia kwa ukalibu elimu tosha Kazi kwangu kuzingatia na kutoa mwongozo kwa mkewangu

    ReplyDelete
  3. Nimepata somo kubwa sana... Mbarikiwe

    ReplyDelete
  4. Asante sana kwa kutuelimisha kuhusu vyakula muhimu naamini nitapata mtoto mwenye afya bora

    ReplyDelete
  5. Ahsante sijatoka sana apo

    ReplyDelete
  6. Asantee kwa elimu nzuri maana akina mama wengi tumezoea kula pasipo kufuata mpangilio maalum, sasa naweza kufuata mlo kamili kwa ajili ya afya ya mtoto na mimi pia.

    ReplyDelete
  7. Asante endeleza elimu ni nzuri

    ReplyDelete
  8. Asante Sana kwa somo zuri nimeelewa na nitalifanyia kazi

    ReplyDelete
  9. Ahsante mke Wang ataniletea mtoto mwenye akili

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA UFAHAMU SIKU ZA KUSHIKA MIMBA

Habari za leo rafiki yangu mpendwa, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia elimu uipatayo hapa pia napenda kuwapongeza wote wachukuao hatua kwa kutumia virutubisho vyetu na wale wanaouliza pale ambapo hawakupaelewa, hii ni kutokana na maoni yenu juu ya kuwafunza jinsi ya kuweza kuhesabu mzunguko wenu wa hedhi kupanga na kuepuka mimba, leo nipo hapa kuwajuza haya. Sasa basi kutokana na wanawake wengi kutokujua mizunguko yao ya hedhi, hivyo huwawia vigumu kujua ni siku gani iliyosahihi ili akutane na mumewe ama aepuke ili kubeba mimba au kutokushika mimba. Ni muhimu sana mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, hii pia itakusaidia kujua siku hatari za kushika mimba na vile vile kukusaidia kuepuka mimba usiyoitarajia kwa kutumia kalenda yako kupanga tarehe yako.  NAMNA YA KUHESABU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI Ili kujua siku nzuri ya kupata mimba au kuepuka ni lazima kwanza ujue siku ya KILELE BUKUKU (productive/fetal day) kwa maana kwamba ujue siku ambayo huitwa SIKU YA KUMI NA...

MKE MWEMA MTU HUPEWA NA BWANA. SIFA ZA MKE MWEMA

SIFA ZA MKE MWEMA 1) Kamwe usinyanyue sauti yako kwa mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara kuwa huna adabu na heshima. Pia niliwahi kufundisha hapa Ndoa Maridhawa kuwa radi haioteshi mazao yetu shambani licha ya kuwa na kelele na sauti kubwa, lakini mvua ambayo haina makelele huotesha mazao yetu shambani. 2) Usitangaze udhaifu wa mumeo kwa familia yako na marafiki zako. Linaweza kukuathiri wewe pia. Wewe ni mtunza siri wa mwenzako, na yeye ni mtunza siri wako. 3) Usitumie mihemko na hisia kali kuwasiliana na mumeo, hujui namna atakavyoitafsiri. Wanawake wenye mihemko iliyopitiliza hawawezi kuwa na ndoa yenye furaha. 4) Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui undani wa maisha ya hao wengine. Ukiishambulia HADHI yake, upendo wake kwako utayeyuka. 5) Usiamiliane vibaya na marafiki wa mumeo kwa sababu tu huwapendi, mtu anayepaswa kuepukana nao ni mumeo. 6) Usisahay kuwa mumeo alikuoa wewe, hakumuoa huyo mfanyakazi wako wa ndani au mtu mwingine. Fany...