Skip to main content

JE WAZIJUA SIRI ZA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA

Hello hellow msomaji wa makala zangu unajua nini...????
Leo nataka nikupe siri za mtindo wa maisha unavyoleta afya njema. Wanadamu ni viumbe kamili. Mara nyingi kile tunachokigawa katika sehemu za kimwili, kiakili, na kiroho ni sehemu za mtu zilizo na uwiano unaoingiliana, wala hazitenganishiki. Kwa maneno mengine, kinachoidhuru akili, kinaudhuru pia mwili.

Kwa mfano watafiti wa kisayansi katika uchunguzi wao uliodhibitiwa wamegundua kwamba kicheko kile kitokanacho na furaha na shangwe huleta mabadiliko yanayoweza kupimwa katika mfumo wa kinga mwilini mwa mtu. Unaweza kabisa kuusaidia mwili wako kupigana na ugonjwa kwa vizuri zaidi ukiwa na furaha! Uchunguzi huo huonyesha jinsi akili na mwili vinavyofanya kazi yao kwa pamoja kwa ushirikiano wa karibu sana.

Jinsi ulivyo ni kutokana na kile unachokula na unachowaza akilini. Hebu tuchambue kidogo ktk maandiko matakatifu, Katika maelfu ya miaka iliyopita Neno la Mungu lilidokeza kuwapo kwa uhusiano huo wenye nguvu kati ya akili na mwili ambao ni hivi karibuni tu umekubaliwa na kuingizwa katika nadharia ya kiganga: “Moyo uliochangamka ni dawa nzuri, bali roho iliyopondeka huikausha mifupa” – (Mithali 17:22).

Kulingana na mtume Yohana, Je, Ni kwa karibu jinsi gani uhusiano huo uliopo kati ya akili na mwili unaathiri usitawi wetu wa kiroho? “Mpenzi wangu, nakutakia mafanikio mema ya kila aina; nakutakia afya njema ya mwili kama ulivyo nayo rohoni” – (3 Yohana 1:2).

Muumbaji wetu anataka sisi tupate ” kufurahia kuwa na afya njema ” Neno la Mungu linaweza kutumika kama chemchem yetu ya afya, pamoja na kuwa chemchem yetu ya uzima wa milele. Kwa kuwa usitawi wetu kimwili na kiakili na kiroho unakwenda bega kwa bega, Paulo anatoa kwetu ombi hili:
“Mlapo mnywapo au mtendapo neno lolote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu” – (1 Wakorintho 10:31).

Injili inajumuisha mambo yote mawili, uponyaji wa mwili na uponyaji wa roho. Mtindo wa maisha uletao afya unaweza kutusaidia sisi kuwa Wakristo wenye uchangamfu mwingi. Hapa zipo kanuni nane za kufuata endapo wewe kweli unataka kuishi maisha yenye afya na yenye manufaa mengi zaidi.

1. Hewa Safi. Hewa safi ya nje, ni ya lazima kwa afya nzuri. Wakati wa mchana na wakati wa kulala usiku, kuingiza na kuitoa hewa kwa njia inayofaa katika nyumba zetu na mahali petu pa kazi hutuhakikishia kwamba damu yetu daima itagawa oksijeni ya kutosha kila sehemu ya mwili wetu. Kuvuta pumzi nyingi wakati wa matembezi ya asubuhi ni njia kuu ya kuupatia mwili wako oksijeni.

Image result for hewa safi

Aina ya hewa tuivutayo ni dhahiri kwamba ni ya maana. Jihadhari usikae mahali penye moshi au mvuke mwingi, penye hewa mbaya au hewa inayochukua vijimea vidogo sana (bacteria) kutoka mahali fulani palipojificha.

Kuvuta tumbako huichafua sana hewa na ni mojawapo ya wauaji wakuu wa siku hizi. Utafiti wa sayansi umethibitisha kuwapo kwa uhusiano unaoleta madhara kati ya tumbako na kansa ya mapafu, ugonjwa wa kuvimba mapafu na kupumua kwa shida ( emphysema) na ugonjwa wa moyo. Mazoea ya mwili kuhusiana na hiyo sumu ya nikotini katika sigareti hufanya uvutaji huo wa sigara (tumbako) uwe mmojawapo wa mazoea magumu kabisa kuachana hayo. Kuvuta tumbako kutaweza kuwaua watu milioni 12 kwa mwaka kufukia mwaka wa 2020 endapo mwendo huu wa sasa utaendelea

2. Mwanga Wa Jua. “Faida za mwanga wa jua ni nyingi:
1. Dakika kumi na tano hadi 30 za kupata mwanga wa jua kila siku katika ile sehemu ya mwanzo ya asubuhi au baadaye mchana alasiri husaidia mwili kukusanya pamoja au kutengeneza Vitamini D yake wenyewe, kirutubisho muhimu/homoni ndani ya ngozi. Vitamini D huisaidia damu kutengeneza kalisi (calcium) na fosforasi, inayoijenga na kuitengeneza mifupa.

Related image

2. Mwanga wa jua unafanya kazi yake kama dawa ya kuvika viini vya maradhi na kuua vijimea vidogo sana (bacteria)3. Jua linatoa nguvu ambayo kwa hiyo mimea inaweza kuigeuza kaboni dioksidi na maji kuwa kabohidreti [chakula cha wanga]… Bila ya njia hiyo wanyama na wanadamu wangekufa kwa njaa 4. Jua pia linamsaidia mwanadamu kujirekebisha na kukabiliana na kazi ya usiku na kupunguza unyong’onyevu (depression) unaotokana na siku za giza wakati majira ya baridi kali yanapotokea.

Neno la tahadhari: Mwanga wa jua unaweza pia kuleta madhara kukaa kwa muda mrefu kwenye mwanga wa jua kunaweza kuiunguza ngozi, kunaweza kuongeza hatari ya kupatwa na kansa ya ngozi kunaweza kuharakisha kuzeeka, kunaweza kuyaharibu macho, na kusababisha mtoto wa jicho (cataracts). ” [Madondoo yote katika Mwongozo huu yamenukuliwa kutoka katika Look up and Live: A Guide to Health, Lesoni ya Watu Wazima, Robo ya kwanza ya mwaka wa 1993, (Nampa, Idaho: Pacific Prexss Publishing Association). Mambo mengi katika Mwongozo huu ambayo hayajawekwa katika Alama za kunukuu yamefundishwa kutoka katika lesoni hiyo hiyo]

3. Kupumzika: Mwili huu ni lazima upumzike ili upate kujitengeneza upya wenyewe. Yatupasa kuwa na muda wa burudani na wa kupumzika ili kupunguza msongo utokanao na kazi pamoja na majukumu ya kifamilia. Bila kuwa na muda wa kutosha kupumzika mara nyingi watu wanakuwa na wasiwasi, mfadhaiko na hasira kali. Msongo huo wa moyo unaweza kuleta ugonjwa ambao utatulazimisha kuchukua pumziko letu ambalo miili yetu ilikuwa inataka kwa muda wote. Hakuna kitu cha badala cha kuweka mahali pa usingizi mzuri wa usiku.

Kuzichaji upya betri zetu za kiroho kwa kuweka utaratibu wa kila siku ni muhimu pia kwa afya yetu ya kimwili. Muda wa kila siku anaotumia Mkristo katika kutafakari, kusoma Biblia, na maombi utaweza kuuponya mwili pamoja na roho. Tunakuhitaji pia kupata pumziko ili kuuvunja mzunguko wa kazi, yaani, kuwa na siku ya kupumzika kila juma, na likizo ya mwaka au nusu mwaka.

4. Mazoezi Ya Mwili: Mazoezi ya mwili ni ya muhimu sana kwa afya yetu: 1. Mazoezi ya mwili husaidia kulirekebisha shinikizo la damu. 2. Mazoezi ya mwili huiruhusu damu nyingi zaidi kuzifikia sehemu zote za mwili na kuifanya mikono na miguu ipate joto. 3. Mazoezi ya mwili yanaondoa mambo yote mawili. Yaani mkazo wa mwili na mfadhaiko wa moyo, na kukusiadia wewe kujisikia vizuri zaidi katika maisha yako. Mazoezi ya mwili kwa kawaida ni tiba bora kabisa ya wasiwasi na msongo (stress).

4. Mazoezi ya mwili hutupatia nguvu ya umeme kwa ajili ya ubongo wetu pamoja na seli za neva. Yanaongeza afya kwa kuuamsha mfumo wa kinga mwilini (immune system). Mwili unapowekwa katika hali ya afya kwa kufanya mazoezi yanayofaa. Ubongo unakuwa na uwezo wa kufikiri kwa ubunifu na ufanisi zaidi. 5. Yanaweza kukusaidia kuiweka vizuri rangi ya uso wako na kukuweka katika hali nzuri kabisa kimwili.

6. Mazoezi ya mwili hukufanya uwe na nguvu nyingi zaidi, hivyo kuchelewesha kupatwa na uchovu kimwili na kimawazo 7. Yanausaidia ubongo wako kutengeneza dawa inayokupa wewe hali ya kujisikia vizuri na kukuongezea uwezo wa kustahimili maumivu.

Endapo wewe ulikuwa hufanyi mazoezi, basi anza taratibu (polepole) na kuongeza nguvu yake hatua kwa hatua upatapo uwezo wa kustahimili. Laweza kuwa ni jambo la busara kumwona mganga wako kabla ya kuanza mazoezi hayo. Lengo lako na liwe kujishughulisha na kila aina ya mazoezi hayo ya mwili ambayo yanaweza kulinganishwa na kutembea maili moja kwa dakika kumi na tano mara nne au zaidi kw ajuma.

5. Maji: Kwa vile maji ni ya lazima kwa kila seli mwilini, basi, ingetupasa kunywa maji mengi. 1. Kwa uzito, mwili wetu karibu asilimia sabini ni maji… 2. Mwili wetu unahitaji takribani visaga (quarts) viwili na nusu vya maji kila siku ili uweze kufanya kazi zake zote. Baadhi ya kazi hizo ni pamoja na mzunguko wa damu mwilini, kuondoa uchafu mwilini, kusafirisha virutubisho vya chakula mwilini, na kukiyeyusha chakula mwilini

Image result for maji

3. Mtu wa kawaida anazo seli za ubongo kati ya billioni 15 na 40 hivi. Kila moja ya hizo ina maji asilimia 70 hadi 85. Maji ya kutosha kuweza kuzigawa seli hizo hukufanya uwe na akili iliyochangamka, halafu husaidia kuzuia mfadhaiko (depression) na hasira kali. 4. Si maji yale tu unayokunywa ambayo ni ya muhimu. Kuoga maji ya baridi kidogo au vuguvuvugu kila siku au kwa kutumia bafu ya manyunyu (shower) huboresha mzunguko wa damu mwilini, hivyo kuupa mwili na ubongo wako nguvu.

Bafu ya manyunyu au kuoga kwa njia ya kawaida huweza pia kutuliza mishipa ya fahamu iliyochachamaa, ambayo inaweza kuleta ugonjwa kwa kudhoofisha mfumo wa kinga mwilini. Kuoga pia kunaondoa uchafu kutoka juu ya ngozi, pia kunaweza kupunguzahoma.

6. Lishe Ifaayo: Wakati ule wa uumbaji Mungu alimwagiza Adamu na Hawa kula chakula cha kokwa, nafaka na matunda (Mwanzo 1:29). Baada ya Adamu na Hawa kutenda dhambi, ziliongezwa mboga za majani katika lishe yao (Mwanzo 3:18). Baada ya ile gharika, Muumbaji aliongeza nyama ya wanyama “safi” katika lishe yao (Mwanzo 7:2-3, 9:1-6).

Nyama ya wanyama (aina yote – kuku, samaki, dagaa, nguruwe, ng’ombe, n.k.) ina mafuta ya majimaji (saturated fat) na mafuta mazito kolestero [cholesterol], ambayo yote huongeza hatari ya kupatwa na shinikizo la damu, kupooza (stroke), ugonjwa wa moyo, kansa, unene usio wa kawaida, kisukari na magonjwa mengineyo. Leo matabibu wengi wanawashauri wale wanaokula nyama kula mnofu ule tu usiokuwa na mafuta, uliopikwa vizuri, pamoja na kula samaki na kufanya hivyo kwa nadra sana.

Kwa vile watu wanaokula chakula cha mimea wana afya bora zaidi, tena wanaishi kwa muda mrefu zaidi, wataalamu wengi wa lishe na afya wanatusihi sana sisi ili tupate kufikiria kukirudia chakula kile cha awali walichopewa wanadamu cha kokwa, nafaka na matunda pamoja na mboga za majani zilizoongezwa.

Ukitaka kuanza kula vyakula vya mimea, ule aina mbalimbali za matunda, pamoja na kokwa [karanga n.k.] nafaka, maharage, kunde, mbaazi na mboga za majani. Mbogamboga (vegetables) kama mboga za majani, mizizi (viazi, karoti, n.k.), n.k. ni muhimu sana. Tumia nafaka (ngano, mchele, n.k.) zisizokobolewa na unga wa nafaka isiyokobolewa badala ya ule iliyokobolewa (mweupe). Acha matumizi yako ya mafuta ya wanyama (samli, siagi, mafuta ya nguruwe, shahamu izungukayo figo, n.k.) na punguza kutumia mafuta ya mimea (alizeti, karanga, zeituni, mawese) au hata uache. Kula kwa kufuata mapendekezo yaliyo juu itasaidia usihitaji mazao ya wanyama (maziwa, mayai, nyama aina zote, kuku, samaki, dagaa, n.k.).

Wale wanaochagua kula nyama kama sehemu ya chakula chao, wangepaswa kuzila nyama zile tu ambazo Biblia inasema ni “safi”au zile zinazofaa kuliwa na wanadamu. Mungu alipowaruhusu wanadamu kula nyama baada ya gharika (Mwanzo 7:2-3; 9:1-6), alibainisha nyama za wanyama gani zilikuwa safi, na zipi zilikuwa najisi na zilikuwa hazifai kuliwa.

Soma katika Mambo ya Walawi 11 na Kumbukumbu la Torati 14 orodha ya ndege, wanyama, na samaki ambao Mungu alisema hawafai kuliwa. Kwa mujibu wa sura hizo, wanyama safi ni lazima kwato zao zigawanyike na pia wacheue. Samaki safi ni lazima wawe na magamba na mapezi, vyote viwili. Ndege wanaokula uchafu ni marufuku kuliwa.

Miongoni mwa wanyama najisi, kwa namna ya pekee nguruwe wanatajwa kwa kulaaniwa (Kumbukumbu la Torati 14:8) Asilimia ya juu ya miili ya wanadamu inayofanyiwa uchunguzi na waganga imejaa minyoo isiyokufa ya trikina (trichinae). Minyoo hiyo midogo sana inahamishiwa kwa wanadamu wale wanaokula nguruwe walioambukizwa minyoo hiyo. Utafiti wa kisanyansi wa siku hizi unazidi kufunua sababu zinazoonyesha kwa nini Mungu alitangaza nyama za wanyama fulani kuwa ni najisi. Sababu moja huenda ikawa ni yale matokeo yanayoleta uharibifu mkubwa kutokana na mafuta ya wanyama ya majimaji katika mfumo wa mwili wa kibinadamu wa kuyeyusha chakula.

7. Epuka Vitu Vinavyoleta Madhara: Je, ni maonyo gani ambayo Biblia inatoa kuhusu vinywaji vyenye alcohol ndani yake? “Mvinyo hudhihaki na kileo huleta ugomvi; Na akosaye kwa vitu hivyo hana hekima” – Mithali 20:1. Wala wezi wala watamanio, wala WALEVI, wala watukanaji hawataurithi ufalme wa Mungu” – (1 Wakorontho 6:10).

Alkoholi huathiri mifumo ya mwili ifuatayo: 1. Mfumo wa kinga mwilini – Alkoholi inapunguza uwezo wa chembechembe nyeupe wa kupigana na ugonjwa, hivyo kuzidisha hatari ya kupatwa na nimonia (pneumonia), kifua kikuu, homa ya manjano, na kansa za aina kadhaa. 2. Mfumo wa tezi (endocrinesystem) zinazotoa majimaji mwilini – Vinywaji viwili tu au vitatu kwa siku huzidisha hatari ya kuharibika mimba, kuzaa watoto waliokufa, na watoto waliozaliwa kabla ya wakati wake.

3. Mfumo wa mzunguko wa damu mwilini Matumizi ya alkoholi huzidisha hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo, hupunguza sukari katika damu, na kuzidisha kiwango cha mafuta katika damu na kuongeza mapigo ya moyo, hivyo kuzidisha shinikizo la damu.4. Mfumo wa kuyeyusha chakula – Alkoholi inaleta kuwasha tumboni, na kwa njia hiyo kusababisha kutoka damu katika tumbo hilo… Mazoea ya kutumia alkoholi huzidisha hatari kwa ini kuw ana mafuta mengi, homa ya manjano, na ugonjwa wa ini (cirrhosis).

Alkoholi inahusika na asilimia kubwa ya watu wanaojiua wenyewe, vifo vinavyosababishwa na magari, kuwatendea vibaya watoto, na ukatili uliomo nyumbani.

8. Kuutumainia Uweza Wa Mungu: Mtu anayesumbuliwa mara kwa mara na hofu au hatia ataona vigumu kwake kupata manufaa kamili kutokana na mazoea hayo ya afya tuliyotoka kuyaeleza muda mfupi tu uliopita. Lakini mtu yule mwenye imani isiyo na shaka kwa Mungu atapata chimbuko hili la mwisho litakalomletea hali njema katika maisha yake.

“Ee nafsi yangu umhimidi BWANA, wala usizisahau fadhili zake zote – yeye anayekusamehe dhambi zako zote na KUKUPONYA MAGONJWA YAKO YOTE, ANAYEUKOMBOA UHAI WAKO na kaburi” – Zaburi 103:2-4.

David Larson, mshauri wa Taasisi ya Taifa ya Afya ya Akiliki kule Marekani, alifanya utafiti wake mpana juu ya uhusiano wa moja kwa moja uliopo kati ya dini na afya.Uchunguzi wake ulionyesha wazi kwamba upo uhusiano wa moja kwa moja kati ya Mkristo aliyejitoa na afya. Alishangaa kujua kwamba, wale wanaohudhuria kanisani wanaishi kwa muda mrefu kuliko wale wasiohudhuria. Wale wanaokwenda kanisani wana upungufu wa kupatwa na mshtuko wa moyo, Mishipa ya arteri kuwa migumu, shinikizo la damu, na magonjwa mengine. Wale wanaomwamini Mungu huishi maisha yenye manufaa zaidi kwa sababu hawapatwi kirahisi na mfadhaiko, hawageuki na kuwa walevi sugu, kufungwa kama wahalifu wanaorudia mle tena na tena, na kunaswa katika ndoa isiyo na furaha. Kuutamainia uweza wa Mungu ndio msingi wa ustawi wa kweli na maisha ya afya yenye furaha.

Waadventista, Wasabato wapatao 50,000 hivi walichunguzwa, hasa kule California kwa kipindi cha zaidi ya miaka 30. Matokeo yalionyesha kwamba Waadventista wanaume wanaishi miaka 8.9 na wanawake miaka 7.5 kuliko watu wengine wote kwa jumla. Uchunguzi huo wa Waadventista kule Uholanzi, Norway na Polandi huonyesha matokeo yanayofanana na hayo. Watafiti wanaona kwamba sababu ya kipindi kirefu cha kuishi kwa Waadventista inatokana na kuzifuata kwao baadhi au kanuni zote nane za afya zilizoelezwa katika mwongozo huu. Wale wanaozifuata kanuni hizi sio tu kwamba wana maisha marefu zaidi, bali pia wana maisha yaliyo bora sana.

Tukiutumia mtazamo wa Biblia katika maisha yetu tutakuwa tofauti katika aina zote za njia za utendaji wetu na kutoa ushahidi unaovutia kuonyesha kwamba katika ulimwengu mzima Ukristo ni dini inayoweza kuwekwa katika vitendo. Inawabadilisha watu – yaani, fikra zao na matendo yao na kujenga mtindo mpya wa maisha.

Kutokana na uhusiano wa karibu sana uliopo kati ya akili, mwili na maisha yetu ya kiroho, Wakristo wale wanaoishi kwa Neno la Mungu watataka kuzifuata kanuni hizo za mtindo wa maisha uletao afya wanapojiandaa kwa ajili ya marejeo yake Yesu (1 Yohana 3: 1-3). Sio tu kwamba Kristo anataka sisi tuwe tayari kukutana naye atakaporudi, pia anataka kuyaboresha maisha yetu ya sasa. Tunaweza kushirikiana naye kwa kuzifuata hizo kanuni za afya za Mungu.

Yesu anaahidi kutuokoa sisi mbali na kila tabia iletayo uharibifu mwilini kwa “kadri ya nguvu [yake] itendayo kazi ndani yetu” (Waefeso 3:20). Endapo wewe unajitahidi kuishinda tabia fulani inayokuathiri mwili wako kama vile kutumia tumbaku au kunywa vileo, basi, maazimio yako hayo mazuri sana ya kutaka kuacha tabia hiyo mara nyingi yanageuka na kuwa kwako kama kamba za mchanga. Lakini kwa kuuchota uwezo wa Mungu unaotenda kazi ndani yako Mungu aweze kukupa wewe nguvu za kukuwezesha kushinda. Neno la Mungu linaahidi hivi: ” Naweza kufanya mambo yote kwa njia yake Kristo anitiaye nguvu” (Wafilipi 4:13).

Contact us +255767962720/0679621470

Comments

Popular posts from this blog

VYAKULA MUHIMU ZAIDI KWA MAMA MJAMZITO

LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NI MUHIMU SANA, KWANI LISHE HII HUTUMIKA KWA MAMA NA MTOTO ANAENDELEA KUKUA TUMBONI. KWA KAWAIDA MAHITAJI YA CHAKULA NA VIRUTUBISHO MWILINI MWA MWANAMKE HUONGEZEKA WAKATI WA UJAUZITO NA KADRI UJAUZITO UNAVYOENDELEA KUKUA, VIRUTUBISHO HIVYO HUTUMIKA KUJENGA MWILI WA MAMA NA MTOTO. HIVYO MAAMUZI YA LISHE AU LISHE MAMA ANAYOPATA HUATHIRI PIA MAENDELEO YA MTOTO ANAYEKUA MWILINI MWAKE. TUTAONA VYAKULA MUHIMU VYA KUZINGATIA LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NA BAADHI YA VITU VYA KUKWEPA. Mama mjazito akipata mlo wenye mboga za majani Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini; Nafaka na Vyakula vya Wanga. Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi iki

UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA UFAHAMU SIKU ZA KUSHIKA MIMBA

Habari za leo rafiki yangu mpendwa, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia elimu uipatayo hapa pia napenda kuwapongeza wote wachukuao hatua kwa kutumia virutubisho vyetu na wale wanaouliza pale ambapo hawakupaelewa, hii ni kutokana na maoni yenu juu ya kuwafunza jinsi ya kuweza kuhesabu mzunguko wenu wa hedhi kupanga na kuepuka mimba, leo nipo hapa kuwajuza haya. Sasa basi kutokana na wanawake wengi kutokujua mizunguko yao ya hedhi, hivyo huwawia vigumu kujua ni siku gani iliyosahihi ili akutane na mumewe ama aepuke ili kubeba mimba au kutokushika mimba. Ni muhimu sana mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, hii pia itakusaidia kujua siku hatari za kushika mimba na vile vile kukusaidia kuepuka mimba usiyoitarajia kwa kutumia kalenda yako kupanga tarehe yako.  NAMNA YA KUHESABU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI Ili kujua siku nzuri ya kupata mimba au kuepuka ni lazima kwanza ujue siku ya KILELE BUKUKU (productive/fetal day) kwa maana kwamba ujue siku ambayo huitwa SIKU YA KUMI NA NNE

Here are some tips for you to work for your picnic and barbecue during pregnancy.

1. Understand the foods to avoid during pregnancy: You can still enjoy most foods, but the main summer foods you should avoid include: Uncooked soft cheese, Marinated meat, Homemade mayonnaise, unless it is made with a lion egg cover (shopped mayonnaise is good), Homemade ice cream is made with lion-capped eggs (again, the ice cream bought at the store is good). 2. Check the grilled meat and fish:  It’s perfectly fine to ridicule the burger on the barbecue when you are pregnant, but just check if the meat is cooked thoroughly. Otherwise, you can get food poisoning from bacteria. Check that the meat in the middle is pink and put the skewer in the thickest part of the meat to make sure the juice is clear. And don't worry about offending the owner by checking: it's important when you are pregnant. If you make your own barbecue, wait until the charcoal is red and have a powdery gray surface before you start cooking. Make sure to use separate utensils and plates for raw and coo