Skip to main content

WANANDOA MPOOO?? NISIKILIZENI KWA MAKINI WANANDOA.

1.UTAMSHANGAA SANA:
Image may contain: one or more people, ocean, beach, water, shoes, sky, outdoor and nature
Mnapooana, hasa baada ya kumpata yule unadhani ni mwenzi halisi na anayekufaa unaamini kwamba utakuwa naye kwa furaha hadi kifo kitakapo watenganisha na utakuwa mtu wa furaha milele.
Ila siku moja utaamka asubuhi na kugundua kwamba hata kama ni mtu maarufu sana duniani bado hawezi kukufanya wewe kuwa mtu wa furaha siku zote na zipo siku utakuwa uajiuliza hivi kwa nini ulikuwa na haraka kumkubali na kuoana naye.
Sasa matarajio yanapotea, unajisikia upweke, na unaaanza kujifunza kwamba ndoa si kituo kufikia baada ya maisha ya kujitafutia mtu wa kuishi naye duniani bali safari iliyojaa raha na karaha kuelekea kujuana na kujenga familia bora na imara.
2.UTAFANYA KAZI KUBWA ZAIDI YA ULIVYOTEGEMEA.
Mapema watu wanapokwambia ndoa ni kazi unadhani labda itakuwa ni kuvumilia kwa kuwa mwenzako anasahau kufanya wajibu wake katika kazi za kila siku ndani ya nyumba.
Na unaamini kwamba hata kama anatabia fulani fulani mbaya basi utamvumilia kwa kuwa unampenda.
Kuoana ni kudhihirisa umemaliza degree ya kwanza sasa unaingia Graduate studies (Masters au Phd) na inahitaji kazi kuliko unavyotegemea.
Ndiyo maana sasa unapambana na matatizo hayo unayopitia kwani inawezekana hukudhani kwamba siku moja utajikuta katika njia panda ambayo unahisi inakuchanganya zaidi.
Hata hivyo bado nafasi unayo na ndoa yako ina uhai mkubwa
3.KUNA WAKATI UTAENDA KULALA OVYO KABISA
Wengi huwashauri wanandoa wapya kwamba “usiende kulala huku umekasirika” kama vile hawajui nini hutokea kwenye vyumba vya kulala vya wanandoa.
Na wengine hujihurumia sana kwa kuwa wapo single eti usingizi ni wa mang'amung'amu wakioa na kuolewa ndipo watalala vizuri vifuani mwa wapenzi wao.
Thubutu! vyumba vingine vya kulala ni kisima cha machozi na kelele za migogoro hadi usiku wa manane hata usingizi hakuna.
Kitu cha msingi ukikasirishwa just come down and be loving endelea na maisha hakuna mtu anaweza kukufanya uwe na furaha isipokwa wewe kwanza..
4.KUNA WAKATI UTAISHI BILA TENDO LA NDOA
Si kwamba siku zote wanandoa huwa na mood kwa ajili ya sex, anaweza kuwa mmoja au wote. Kukosa mood au sex drive ni sehemu ya maisha ya ndoa na hii haina maana kwamba hutataka sex tena bali ni kipindi kutokana na maisha yanavyoenda.
Kitu cha msingi ni kwamba hata kama hamfanyi basi kunatakiwa kuwepo na romantic life kama vile touching, kissing, hugging.
Hivyo ingia kwenye ndoa ukijua sex si chakula bali hitaji la mwili kwa ajili ya kuridhishana wawili wanaoishi pamoja.
5.NDOA IMARA HAINA MAANA HAKUNA MIGOGORO
Kubishana au kupingana au kupishana kimawazo au jambo lolote ni sehemu ya maisha ya ndoa.
Pia ni njia nzuri ya kujuana na kuwekana sawa tena hili inabidi lifanywe kwa upendo pia kuvumiliana na kuyamaliza ndani ya dakika 15

Comments

Popular posts from this blog

MFAHAMU MWANAMKE KIUNDANI NA ANACHOKIPENDA

Katika mapenzi wanawake wanapenda ufanye kile wanachokitaka japo ni vigumu kujua mwanamke anapenda nini. Kwa hiyo kama ni vigumu kujua kitu gani anapenda basi ni vizuri kuwa makini na kugundua ni kitu gani hapendi ili usimfanyie ambacho hapendi na ufanye anachopenda. Japokuwa si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu.  Kwa sababu hiyo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini  na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha. Kisha fanye vile wanavyovipenda. Hiki ni kimojawapo Hupendela tendo la ndoa lidumu muda mrefu. Wanawake hupenda tendo la ndoa lidumu walau kwa dakika mbili. Na wanatamani ikiwezekana hata ikibidi ifanyike siku nzima. Sio muda tuu ndio muhimu bali hata kile unachofanya. Wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wakae muda mrefu katika tendo, lakini kutokana na tafiti hili sio sababu, wanawake wengi hupenda zaidi...

JE WAZIJUA SIRI ZA MTINDO WA MAISHA ULETAO AFYA

Hello hellow msomaji wa makala zangu unajua nini...???? Leo nataka nikupe siri za mtindo wa maisha unavyoleta afya njema. Wanadamu ni viumbe kamili. Mara nyingi kile tunachokigawa katika sehemu za kimwili, kiakili, na kiroho ni sehemu za mtu zilizo na uwiano unaoingiliana, wala hazitenganishiki. Kwa maneno mengine, kinachoidhuru akili, kinaudhuru pia mwili. Kwa mfano watafiti wa kisayansi katika uchunguzi wao uliodhibitiwa wamegundua kwamba kicheko kile kitokanacho na furaha na shangwe huleta mabadiliko yanayoweza kupimwa katika mfumo wa kinga mwilini mwa mtu. Unaweza kabisa kuusaidia mwili wako kupigana na ugonjwa kwa vizuri zaidi ukiwa na furaha! Uchunguzi huo huonyesha jinsi akili na mwili vinavyofanya kazi yao kwa pamoja kwa ushirikiano wa karibu sana. Jinsi ulivyo ni kutokana na kile unachokula na unachowaza akilini. Hebu tuchambue kidogo ktk maandiko matakatifu, Katika maelfu ya miaka iliyopita Neno la Mungu lilidokeza kuwapo kwa uhusiano huo wenye nguvu kati ya akili n...

Je unajua kuwa Ndoa Imara Huweza Kutibu Hata Kansa:

Maradhi ya kansa yamekuwa yakiwasumbua watu wengi sana kwa nyakati za hivi karibuni. Hata hivyo kuna aina nyingi za kansa, mojawapo ni ile ya kibofu cha mkojo. Kulingana na utafiti mmoja uliofanywa nchini marekani, imeonesha kwamba, msaada wa karibu unaotolewa na wanandoa kwa wanandoa wenzao ambao, wameathirika na ugonjwa wa kansa ya kibofu cha mkojo, ni aina mojawapo ya tiba inayoweza kuwafanya wagonjwa hao wajisikie vizuri na kuishi kwa muda mrefu. Utafiti huo ulionyesha kwamba, watu wanaougua ugonjwa huo ambao wako kwenye ndoa, wana nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu zaidi ukilinganisha na wenzao ambao hawajaoa au kuolewa. Hali hii haichagui umri, rangi au hata kiwango cha athari ya ugonjwwa wenyewe. Ndoa Imara Huweza Kutibu Hata Kansa. Vilevile, tafiti mbalimbali za huko nyuma ziliwahi kuonesha kwamba, ndoa bora na imara zina uwezo wa kuwaongezea ahueni wanandoa wanaougua maradhi ya kansa ya matiti na ile ya mkojo. Watafiti hao walizidi kusema kwamba utafiti huo mpya unaweza ...