Skip to main content

UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA UFAHAMU SIKU ZA KUSHIKA MIMBA

Habari za leo rafiki yangu mpendwa, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia elimu uipatayo hapa pia napenda kuwapongeza wote wachukuao hatua kwa kutumia virutubisho vyetu na wale wanaouliza pale ambapo hawakupaelewa, hii ni kutokana na maoni yenu juu ya kuwafunza jinsi ya kuweza kuhesabu mzunguko wenu wa hedhi kupanga na kuepuka mimba, leo nipo hapa kuwajuza haya.
Sasa basi kutokana na wanawake wengi kutokujua mizunguko yao ya hedhi, hivyo huwawia vigumu kujua ni siku gani iliyosahihi ili akutane na mumewe ama aepuke ili kubeba mimba au kutokushika mimba. Ni muhimu sana mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, hii pia itakusaidia kujua siku hatari za kushika mimba na vile vile kukusaidia kuepuka mimba usiyoitarajia kwa kutumia kalenda yako kupanga tarehe yako.

 NAMNA YA KUHESABU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
Ili kujua siku nzuri ya kupata mimba au kuepuka ni lazima kwanza ujue siku ya KILELE BUKUKU (productive/fetal day) kwa maana kwamba ujue siku ambayo huitwa SIKU YA KUMI NA NNE. Rafiki napenda mtambue kuwa wanawake mnatofautiana katika swala la urefu wa mzunguko wa hedhi (menstrual periods) yani idadi ya siku ya kwanza ya period mpaka hedhi ya pili, wanawake wengi huwa mnaangukia Kwenye tarehe 22-35 ingawa wapo walio kawaida wanachukua siku 28

Vilevile wengine Wana mizunguko miwili yani mfupi na mrefu hivyo walio na mzunguko mfupi mathalani wale wenye siku 22 huwa Wana kipindi kifupi cha utokaji damu yan damu inaweza kukatika ndani ya siku mbili huwa ni tofaut na mtu mwenye mzunguko wa siku 31- 35 kwani wao huwa na kipindi kirefu cha utokaji damu.

JE, UNAIJUA SIKU YA MIMBA???
watu wengi huwa hatujui  na kuishia kuchemka katika swala hili la mzunguko wa hedhi na kutambua siku ya mimba ni ipi wao hufikiri siku ya mimba ni Ile siku ya kumi na nne baada ya Dalili za kwanza za damu, wao huhesabu kuanzia Ile siku damu ilipoanza kutoka hadi siku ya kumi na nne, kwa utaratbu huu wengi wanaanguka hii ni kwasababu wanawake Wana mizunguko tofauti kwa urefu hivyo basi nakuelekeza ili ujue siku ya mimba ni ipi

Kwanza inabid ujue mzunguko wako ni upi??? Yan mfupi /mrefu /wa kawaida. Baada ya kujua urefu wa mzunguko wako chagua (pin - point) yani siku Ile ya mwisho halafu uhesabu kurudi nyuma (backwards) siku kumi na tano kuanzia siku Ile ya mwisho yani siku kumi na tano kuanzia mwisho ndio siku ya mimba, hapa namaansha ukishafahamu siku ya kumi na tano kutoka mwisho hukuwezesha kufaham siku ya kupata ujauzito

Kwa utaratibu huu mdogo msomaji utagundua karibia wanawake wote au wewe mwenyewe unatumia njia za Zaman ambazo huwafaa watu wenye mzunguko wa siku 28 tu hivyo nakupa mifano Hai jinsi ya kutumia kalenda kwa mizunguko yote.

MZUNGUKO WA SIKU 28
Image may contain: text
Tengeneneza kalenda yako ya siku 28 yani hivi 1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,14,15,16,17,18,19,20,21,22,23,24,25,26,27,28
Baada ya kuandaa hesabu kuanzia 28 mpaka siku ya kumi na tano ambayo itaangukia Kwenye (14th) day sasa hiyo ndio siku ya kubeba mimba kwa mwanamke yoyote mwenye mzunguko wa siku 28 Lakin kwakua kipindi cha ovulation kinaanza siku ya 4-5 kabla ya ovulation na humalizika masaa 24-48 hivyo unapaswa kujikinga kuanzia tareh 12-16 kuepuka mimba hii ni kwasababu mbegu za mwanaume Zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24-48 baada ya kujamiiana,
kumbuka :siku ya kwanza ndio siku unayoanza kubreed

MZUNGUKO WA SIKU 22
 Tengeneneza kalenda yako ya siku 22 yani hivi
1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,14,15,16,17,18,19,20,21,22, Baada ya kuandaa hesabu kuanzia 22 kurudi nyuma mpaka siku ya kumi na tano ambayo itaangukia Kwenye (8th)hivyo siku hiyo ni siku ya hatari kubeba mimba ila kwa kuangalia ovulation inabid ujikinge kuanzia tarehe 6-10 kuepuka mimba hii ni kwasababu mbegu za mwanaume Zina uwezo wa kudumu kwa muda wa masaa 24-48 kumbuka tareh moja ndio siku unayoanza kubreed

MZUNGUKO WA SIKU 35
No photo description available.
Tengeneneza kalenda yako ya siku 35 yani kama hivi
1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,14,15,16,17,18,19,20,21,22,23,24,25,26,27,28,29,30,31,32,33,34,35. Baada ya kuandaa hesabu kuanzia 35 kurudi nyuma mpaka sku ya kumi na tano ambayo itaangukia Kwenye (21th)hivyo hiyo siku ni ya hatar kubeba mimba ila kutokana na ovulation inabid uanze kujizuia kuanzia tareh,19-23 kuepuka mimba hii ni kwasababu mbegu za mwanaume Zina uwezo wa kudumu kwa masaa 24-48 baada ya kujamiiana

MZUNGUKO USIO WA KAWAIDA WA SIKU KUMI NA TANO
Mara nyingi Watu Hawa huwa na mzunguko wa siku 15-18 Hawa huwa na wa kutokushika mimba hivyo kwanza tengeneneza mzunguko wa siku zako
1,2,3,4,5,6,7,8,9,10,11,12,13,14,15 Kisha Anza kuhesabu kuanzia 15 kurudi nyuma mpaka ufike siku kumi na tano. Bila Shaka itaangukia Kwenye (1st) hivyo siku ya kwanza ya mzunguko wa mwanamke yoyote mwenye mzunguko wa siku 15 ndio siku hyo mimba inaingia (hata wa siku kumi na nane follow above) kumbuka siku ya kwanza ndio siku unayoanza kubreed pia ndio siku hiyo unaweza kupata mimba hii inamaanisha kwamba siku ambayo linaharibika lile yai la kwanza ndio siku hyo hiyo yai la upande wa pili linapevuka na kuwa tayari kurutubishwa, Mara nyingi mwanamke wa kundi hili anaweza kupata mimba kama atakutana na mwanaume wake siku Ile anayoanza hedhi kwani ni siku ambayo yai linaharibika na ndio siku hyo yai moja linapevuka na kuwa tayari kurutubishwa

 Mara nyingi wanawake wa kundi hili huwa hawapati ute wa Uzazi ambao wenzao huwa wanapata siku Ile yai linapevuka wao hupata ute uliochanganyikana na damu kwakua ndio siku hyo ya kuanza breed

Ndugu yangu ni matumaini yangu umejifunza na kuelewa jinsi ya kupanga kupata mimba au kuepuka nimeamua kuandaa somo hili ili kupunguza utoaji wa mimba na madhara wanayoyapata wanawake wanaotumia vidonge vya Uzazi wa mpango hivyo ni vizuri KUTUMIA KALENDA ILI KUEPUKANA NA MADHARA YA SINDANO NA VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO AMBAYO NI MAKUBWA KAMA VILE KUPATA SARATAN YA MATITI, KUWA MGUMBA, KUPATA UVIMBE KATIKA KIZAZI, HUSABABISHA KUBLEED SANA NK.

Asante kwa kusoma  kupata elimu hii na wewe unaweza kuwafundisha wenzako kwa kushare hii post na kuwatag marafiki zako. Jipatie virutubisho vya kutibu magonjwa tabia na sugu kama presha,asthma,joint maumivu ya viungo, kuongeza kinga yako, vidonda vya tumbo, alleji na kadhalika usisite kunitafuta.

NOTE: NDUGU MSOMAJI KAMA UNA MAONI USHAURI NIANDIKIE UJUMBE KUPITIA NAMBA YANGU HAPO CHINI 0621746838 AU 0767962720 WHATSAPP


No photo description available.

Comments

  1. Huo ute wa uzazi una mwonekano gani???

    ReplyDelete
  2. Mm naomba nielekezwe jinc ya kuhesabu kalenda mana nikiambiwa cku 22 cku 28 cku 35 nakua cja elewa ukuizo zmepatkana vp

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hesabu ile period yàko ya mwanzo tarehe iliyo anza period..Hadi tarehe ya mwezi unawo fata iliyopata period utajua mzunguko wako ni wa siku ngapi

      Delete
  3. Nimeelewa kwahiyo mwenye mzunguko wa siku 27 siku ya mimba ni 13

    ReplyDelete
  4. Asante kwa somo zuri ,ila mm nashindwa kujua jins Ya kuhesabu mzunguko wangu kwa mfano mm naingia period tar 4mwez huu sasa siku Ya hatar inakuwa lini??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Inamaanisha inabid ujue mzunguko wako huwa na siku ngapi, kama ni 28 jua siku ya nwanza ni tarehe 4, hesabu siku 15 kuanzia siku ya mwisho yaani ya 28 kuja nyuma

      Delete
    2. Inamaanisha inabid ujue mzunguko wako huwa na siku ngapi, kama ni 28 jua siku ya nwanza ni tarehe 4, hesabu siku 15 kuanzia siku ya mwisho yaani ya 28 kuja nyuma

      Delete
  5. Unanza kuhesabu siku Ya kuanza period au mwisho period

    ReplyDelete
  6. Samahan nashukulu kwa darasa lako nimefulai naomba kuhuliza Kama mm naingia 25 mzunguko wangu Ni upi yaan nashindwa kuerewa huwa zinachanganikana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Jua kwanza unaenda siku ngapi ndo kinachomaanishwa

      Delete
  7. Natafuta mtoto myaka mungu nashindwa kutumia kalenda nisaidien jaman

    ReplyDelete
  8. Naomba kuuliza mimi toka nilipo ziona siku zang December 8 adi leo tuko na January 19 cjaona tena apo nakuwa na wasi wasi kwli

    ReplyDelete
  9. Samahani mie sijaelewabado siku zangu huwa hazieleweki Mara 32 Mara 26 na 28 je hapo siku ya kushika ujauzito no ipi? Na natabikia mtt

    ReplyDelete
  10. Mm uwa n 33/35 nmeingia trh 17/2 danger n tareh ngapi

    ReplyDelete
  11. Mm naomba kujua pia mizunguko wangu ni siku 28 ila naingia period siku moja tu kwa mwezi sasa siku ya hatarii itakuwa hiyo hiyo kuanzia 12

    ReplyDelete
  12. Kuna mtu anaingia tarehe 7 kila mwezi siku ya kushika mimba ni siku ipi kwake , naomba kusaidiwa

    ReplyDelete
  13. Asant mwarm me Nina tatizo ra mzunguk was henzi inaweza kupita hats miezi mitatu ndo naina sikuzangu Nina miaka mitatu na nusu nkenyendoa rakn sijaway kupat mimba naitak msaada

    ReplyDelete
  14. Ahsante kwa SoMo, ila samahan. Kama huna mzunguko unaoeleweka je, utajuaje siku ya hatari??

    ReplyDelete
  15. Naomba kuuliza mm nimeingia sku trh 28.10 mpka trh 1.11 mwaka huu 2021 mzunguko wangu ni sku 28 naomba kujua sku Salam na atr

    ReplyDelete
  16. Mm naomba kuuliza ipo mizunguko mingapi ya hedhi au nikuanzia 22 had 36

    ReplyDelete
  17. Namaanisha kuna mwenye mzunguko wasiku 28 27 hadi 36 ipo mingapi

    ReplyDelete
  18. Kuna mdada ameanza period tarehe15 january na amekutana na mtu wake tarehe29-30 je anauwezekano wa kupata mimba na anamzunguko wa siku28

    ReplyDelete
  19. Hi mi huwa naenda period siku 7 ndajuaje mzunguko wangu

    ReplyDelete
  20. Naomba kuuliza period huwa naanza tarehe 20 inarudi tarehe 16 nitajuaje mzunguko wangu

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

VYAKULA MUHIMU ZAIDI KWA MAMA MJAMZITO

LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NI MUHIMU SANA, KWANI LISHE HII HUTUMIKA KWA MAMA NA MTOTO ANAENDELEA KUKUA TUMBONI. KWA KAWAIDA MAHITAJI YA CHAKULA NA VIRUTUBISHO MWILINI MWA MWANAMKE HUONGEZEKA WAKATI WA UJAUZITO NA KADRI UJAUZITO UNAVYOENDELEA KUKUA, VIRUTUBISHO HIVYO HUTUMIKA KUJENGA MWILI WA MAMA NA MTOTO. HIVYO MAAMUZI YA LISHE AU LISHE MAMA ANAYOPATA HUATHIRI PIA MAENDELEO YA MTOTO ANAYEKUA MWILINI MWAKE. TUTAONA VYAKULA MUHIMU VYA KUZINGATIA LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NA BAADHI YA VITU VYA KUKWEPA. Mama mjazito akipata mlo wenye mboga za majani Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini; Nafaka na Vyakula vya Wanga. Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi iki

Here are some tips for you to work for your picnic and barbecue during pregnancy.

1. Understand the foods to avoid during pregnancy: You can still enjoy most foods, but the main summer foods you should avoid include: Uncooked soft cheese, Marinated meat, Homemade mayonnaise, unless it is made with a lion egg cover (shopped mayonnaise is good), Homemade ice cream is made with lion-capped eggs (again, the ice cream bought at the store is good). 2. Check the grilled meat and fish:  It’s perfectly fine to ridicule the burger on the barbecue when you are pregnant, but just check if the meat is cooked thoroughly. Otherwise, you can get food poisoning from bacteria. Check that the meat in the middle is pink and put the skewer in the thickest part of the meat to make sure the juice is clear. And don't worry about offending the owner by checking: it's important when you are pregnant. If you make your own barbecue, wait until the charcoal is red and have a powdery gray surface before you start cooking. Make sure to use separate utensils and plates for raw and coo