Skip to main content

VYAKULA MUHIMU ZAIDI KWA MAMA MJAMZITO

LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NI MUHIMU SANA, KWANI LISHE HII HUTUMIKA KWA MAMA NA MTOTO ANAENDELEA KUKUA TUMBONI. KWA KAWAIDA MAHITAJI YA CHAKULA NA VIRUTUBISHO MWILINI MWA MWANAMKE HUONGEZEKA WAKATI WA UJAUZITO NA KADRI UJAUZITO UNAVYOENDELEA KUKUA, VIRUTUBISHO HIVYO HUTUMIKA KUJENGA MWILI WA MAMA NA MTOTO. HIVYO MAAMUZI YA LISHE AU LISHE MAMA ANAYOPATA HUATHIRI PIA MAENDELEO YA MTOTO ANAYEKUA MWILINI MWAKE. TUTAONA VYAKULA MUHIMU VYA KUZINGATIA LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NA BAADHI YA VITU VYA KUKWEPA.
Related image
Mama mjazito akipata mlo wenye mboga za majani
Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini;

Nafaka na Vyakula vya Wanga.
Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka mbalimbali(mahindi,mtama,ulezi n.k), viazi, ndizi, mihogo. Ni vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili(whole grains) kama mahindi, ngano na mchele usiokobolewa; cereals n.k.cereals

Nyama, Samaki na Vyakula vya Protini.
Hivi ni muhimu kwenye kuujenga mwili, hasa kipindi cha miwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya mtoto vinajengwa. Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri. Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi, senene, panzi na wanyama wengine ; vyanzo vya protini za mimea kama maharage, soya, njugu, njegere, karanga,korosho n.k . Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo vingine vya protini muhimu.vaykula vya protini maziwa

Vyakula vya Mafuta.
Hutumika kwenye kuupatia mwili nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili. Mara nyingi vyakula kama nyama, karanga, ufuta, alizeti,senene, panzi, samaki na matunnda kama maparachichi huwa na mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza mafuta yenye lehemu(cholesterol) nyingi.

Mboga za Majani na Matunda.
Matunda na mboga za majani ni sehemu muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula. Vitamini husaidia kuimarisha kinga ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili. Madini kama ya chuma, kalsiamu, zinki, madini joto(Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto tumboni mwa mama.mboga za majani Vitamini B9 (Foliki asidi) na madini ya chuma hutolewa kama virutubisho ziada kliniki wakati wa ujauzito ili kutosheleza mahitaji ya mwili na kuzuia hatari ya upungufu wa damu kutokea.matunda

Maji
Maji ni muhimu kwenye mmenyenyo na unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya lita 2.3 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, soda, au maji yenyewe. Ni vema zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda.

Mfano wa Mpangilio wa Mlo.
Ili kuhakikisha mlo kamili mjamzito anaweza kufuata mfano wa mpangilio wa mlo ufuatao;

Mfano,
Mlo wa Asubuhi: A - Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi, B - Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua,Uji C - Karoti D - Mayai, E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya
Mlo wa Mchana: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa, B - Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi C - Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya Soya.
Mlo wa Usiku: A - Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa, B - Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati C - Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji, D - Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa E - Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya Soya.
Vitu na Vyakula vya kuepuka/kupunguza
Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto. Haishauriwi kutumia pombe kabisa!
Uvutaji Sigara
Kupunguza unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.
Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi amabayo ni mbaya kwa afya.

Comments

  1. Nashukuru kwa kutufahamisha kumbe sijatoka sana nje na mpangilio wa chakula nnavomuhudumia mkewangu mjamzito

    ReplyDelete
  2. Asantee saana nawafatilia kwa ukalibu elimu tosha Kazi kwangu kuzingatia na kutoa mwongozo kwa mkewangu

    ReplyDelete
  3. Nimepata somo kubwa sana... Mbarikiwe

    ReplyDelete
  4. Asante sana kwa kutuelimisha kuhusu vyakula muhimu naamini nitapata mtoto mwenye afya bora

    ReplyDelete
  5. Ahsante sijatoka sana apo

    ReplyDelete
  6. Asantee kwa elimu nzuri maana akina mama wengi tumezoea kula pasipo kufuata mpangilio maalum, sasa naweza kufuata mlo kamili kwa ajili ya afya ya mtoto na mimi pia.

    ReplyDelete
  7. Asante endeleza elimu ni nzuri

    ReplyDelete
  8. Asante Sana kwa somo zuri nimeelewa na nitalifanyia kazi

    ReplyDelete
  9. Ahsante mke Wang ataniletea mtoto mwenye akili

    ReplyDelete

Post a Comment

Popular posts from this blog

Here are some tips for you to work for your picnic and barbecue during pregnancy.

1. Understand the foods to avoid during pregnancy: You can still enjoy most foods, but the main summer foods you should avoid include: Uncooked soft cheese, Marinated meat, Homemade mayonnaise, unless it is made with a lion egg cover (shopped mayonnaise is good), Homemade ice cream is made with lion-capped eggs (again, the ice cream bought at the store is good). 2. Check the grilled meat and fish:  It’s perfectly fine to ridicule the burger on the barbecue when you are pregnant, but just check if the meat is cooked thoroughly. Otherwise, you can get food poisoning from bacteria. Check that the meat in the middle is pink and put the skewer in the thickest part of the meat to make sure the juice is clear. And don't worry about offending the owner by checking: it's important when you are pregnant. If you make your own barbecue, wait until the charcoal is red and have a powdery gray surface before you start cooking. Make sure to use separate utensils and plates for raw and coo

Vidokezo 10 vya kufurahia barbeque au pikiniki wakati wa ujauzito

Hapa kuna vidokezo kadhaa vya kufanya pikiniki au BBQ zifanyie kazi wakati ukiwa ni mjamzito 1. Jua ni vyakula vipi vya kuzuia ukiwa mjamzito. Bado unaweza kufurahiya vyakula vingi lakini vyakula muhimu vya msimu wa joto ambavyo unapaswa kujiepusha ni pamoja na: jibini laini lisilopikwa, kuponya nyama, mayonnaise ya nyumbani isipokuwa imetengenezwa na mayai makubwa ya simba (mayonesi iliyonunuliwa duka ni sawa), ice cream ya nyumbani isipokuwa imetengenezwa na mayai makubwa ya simba (tena, barafu-iliyonunuliwa duka ni sawa). 2. Angalia nyama iliyochongwa na samaki . Ni sawa kabisa kumdhihaki Burger kwenye barbeque wakati una mjamzito, lakini angalia ikiwa nyama imepikwa vizuri. Vinginevyo, unaweza kupata sumu ya chakula kutoka kwa bakteria. Angalia kuwa nyama iliyo katikati ni nyekundu na weka skewer kwenye sehemu nene ya nyama ili kuhakikisha juisi iko wazi. Na usijali kuhusu kumkosea mmiliki kwa kuangalia: ni muhimu wakati wewe ni mjamzito. Ikiwa utatengeneza barbeque yako m