Skip to main content

MKE MWEMA MTU HUPEWA NA BWANA. SIFA ZA MKE MWEMA



SIFA ZA MKE MWEMA
Image may contain: 1 person, standing
1) Kamwe usinyanyue sauti yako kwa mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara kuwa huna adabu na heshima. Pia niliwahi kufundisha hapa Ndoa Maridhawa kuwa radi haioteshi mazao yetu shambani licha ya kuwa na kelele na sauti kubwa, lakini mvua ambayo haina makelele huotesha mazao yetu shambani.
2) Usitangaze udhaifu wa mumeo kwa familia yako na marafiki zako. Linaweza kukuathiri wewe pia. Wewe ni mtunza siri wa mwenzako, na yeye ni mtunza siri wako.
3) Usitumie mihemko na hisia kali kuwasiliana na mumeo, hujui namna atakavyoitafsiri. Wanawake wenye mihemko iliyopitiliza hawawezi kuwa na ndoa yenye furaha.
4) Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui undani wa maisha ya hao wengine. Ukiishambulia HADHI yake, upendo wake kwako utayeyuka.
5) Usiamiliane vibaya na marafiki wa mumeo kwa sababu tu huwapendi, mtu anayepaswa kuepukana nao ni mumeo.
6) Usisahay kuwa mumeo alikuoa wewe, hakumuoa huyo mfanyakazi wako wa ndani au mtu mwingine. Fanya kutekeleza majukumu yako.
7). Usimpe mtu mwingine jukumu la kumhudumia mumeo. Watu wengine wanaweza kufanya mambo mengine, lakini mumeo ni jukumu lako mwenyewe.
8). Usimshutumu na kumlaumu mumeo akija nyumbani bila kitu. Badala yake mpe hamasa na kumshajiisha.
9). Usiwe mke mbadhirifu, jasho la mumeo ni kitu ghali kabisa ambacho hakipaswi kutupwa hovyo.
10). Usijifanye kuwa unaumwa kwa lengo la kumnyima mumeo tendo la ndoa. Mpe anapotaka. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa wanaume, ni miongoni mwa MAHITAJI MAKUU 3 YA MWANAUME. Ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla mwanamke mwingine hajachukua jukumu hilo. Hakuna mwanaume anayeweza kuhimili vishindo vya ukame
11). Usimjibu mumeo katika uchangiaji wa maoni ya mbele ya umma, muaje ajibu swali lililoelekeza kwake. Ni muhimu usimpinge hadharani mbele ya watu.
12). Usimfokee au kumpinga mumeo mbele ya watoto. Wanawake wenye hekma na busara hawafanyi hivyo.
13). Usishau kuangalia kama mumeo amependeza na amevaa vizuri kabla hajatoka.
14). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mumeo.
15). Usiwe na haraka unapokuwa bafuni na unapojipamba. Huko nje mumeo anakutana na wanawake ambao hutumia muda wa kutosha kujipamba.
16).Wazazi, ndugu an marafiki hawana uamuzi wa mwisho kwenye ndoa yako. Usipoteze muda kuwataka wakupe uamuzi wa mwisho.
17). Usijenge upendo wako kwenye pesa na vitu. Kwa sababu ukiwa na pesa nyingi kumzidi hutoweza kumtii na kumheshimu.
18). Usisahau kuwa mumeo anahitaji mtu wa kumakinika naye na mwenye kumsikiliza, usiwe bize sana kiasi cha kutomtilia maanani. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa kila nyumba yenye furaha.
19). Kama wazo lako limefanya vizuri kuliko la kwake, usifanye ulinganisho wa kujilinganisha naye. Daima mnatakiwa kufanya kazi kama timu.
20). Usiwe mtu wa kumhukumu sana mumeo. Hakuna mwanaume anayempenda mwanamke msumbufu.
21). Mke mvivu huwa na tabia ya kupuuza. Hata hajui kuwa mwili wake unahitaji maji ya kuoga.
22). Je, mume anapenda aina ya chakula unachopika? Jaribu kubadilisha mapishi. Hakuna mwanaume anayefanya mzaha kwenye suala la chakula.
23). Usiwe mtaka makuu kwa mumeo, furahia kila muda na kila kinachopatikana.
24). Ifanye glasi ya maji kuwa ukaribisho nambari 1 kwa mumeo na kila mgeni anayekuja nyumbani kwenu. Mwenendo mzuri ndio urembo wa kweli.
25). Usisuhubiane na wanawake ambao wana mtazamo wa kimakosa kuhusu ndoa.
26). Ndoa yako itakuwa na thamani kadiri unavyoipa thamani. Uzembe haukubaliki.
27). Watoto wako ni baraka kubwa kutoka kwa Mungu, wapende na uwape malezi mazuri.
28). Endelea kutengeneza ushawishi wako ndani ya nyumba yako hata kama una muda mrefu katika ndoa. Usipunguze mapenzi yako kwa familia yako kwa sababu yoyote ile.
30). Mke anayefanya ibada anakuwa amejiimarisha vizuri. Daima muombee mumeo na familia yenu.
Wapo watakaochukia lakini kama umeipenda Like na comment kisha ni follow kila siku

Comments

Popular posts from this blog

MFAHAMU MWANAMKE KIUNDANI NA ANACHOKIPENDA

Katika mapenzi wanawake wanapenda ufanye kile wanachokitaka japo ni vigumu kujua mwanamke anapenda nini. Kwa hiyo kama ni vigumu kujua kitu gani anapenda basi ni vizuri kuwa makini na kugundua ni kitu gani hapendi ili usimfanyie ambacho hapendi na ufanye anachopenda. Japokuwa si wanawake wote wanaweza kukwambia ni nini hasa kinawauzi, kuogopa kukuudhi, hivyo inawafanya wapate shida sana na kuweka maisha yao yawe magumu.  Kwa sababu hiyo wewe kama mwanaume unapaswa kuwa makini  na matendo yao ili kujua tofauti ya vitu ambavyo hawapendi na vile vinavyowapa furaha. Kisha fanye vile wanavyovipenda. Hiki ni kimojawapo Hupendela tendo la ndoa lidumu muda mrefu. Wanawake hupenda tendo la ndoa lidumu walau kwa dakika mbili. Na wanatamani ikiwezekana hata ikibidi ifanyike siku nzima. Sio muda tuu ndio muhimu bali hata kile unachofanya. Wanaume wengi kujali kujizuia, ilimradi wakae muda mrefu katika tendo, lakini kutokana na tafiti hili sio sababu, wanawake wengi hupenda zaidi...

Je unajua kuwa Ndoa Imara Huweza Kutibu Hata Kansa:

Maradhi ya kansa yamekuwa yakiwasumbua watu wengi sana kwa nyakati za hivi karibuni. Hata hivyo kuna aina nyingi za kansa, mojawapo ni ile ya kibofu cha mkojo. Kulingana na utafiti mmoja uliofanywa nchini marekani, imeonesha kwamba, msaada wa karibu unaotolewa na wanandoa kwa wanandoa wenzao ambao, wameathirika na ugonjwa wa kansa ya kibofu cha mkojo, ni aina mojawapo ya tiba inayoweza kuwafanya wagonjwa hao wajisikie vizuri na kuishi kwa muda mrefu. Utafiti huo ulionyesha kwamba, watu wanaougua ugonjwa huo ambao wako kwenye ndoa, wana nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu zaidi ukilinganisha na wenzao ambao hawajaoa au kuolewa. Hali hii haichagui umri, rangi au hata kiwango cha athari ya ugonjwwa wenyewe. Ndoa Imara Huweza Kutibu Hata Kansa. Vilevile, tafiti mbalimbali za huko nyuma ziliwahi kuonesha kwamba, ndoa bora na imara zina uwezo wa kuwaongezea ahueni wanandoa wanaougua maradhi ya kansa ya matiti na ile ya mkojo. Watafiti hao walizidi kusema kwamba utafiti huo mpya unaweza ...

VYAKULA MUHIMU ZAIDI KWA MAMA MJAMZITO

LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NI MUHIMU SANA, KWANI LISHE HII HUTUMIKA KWA MAMA NA MTOTO ANAENDELEA KUKUA TUMBONI. KWA KAWAIDA MAHITAJI YA CHAKULA NA VIRUTUBISHO MWILINI MWA MWANAMKE HUONGEZEKA WAKATI WA UJAUZITO NA KADRI UJAUZITO UNAVYOENDELEA KUKUA, VIRUTUBISHO HIVYO HUTUMIKA KUJENGA MWILI WA MAMA NA MTOTO. HIVYO MAAMUZI YA LISHE AU LISHE MAMA ANAYOPATA HUATHIRI PIA MAENDELEO YA MTOTO ANAYEKUA MWILINI MWAKE. TUTAONA VYAKULA MUHIMU VYA KUZINGATIA LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NA BAADHI YA VITU VYA KUKWEPA. Mama mjazito akipata mlo wenye mboga za majani Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini; Nafaka na Vyakula vya Wanga. Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi iki...