Skip to main content

Je unajua kuwa Ndoa Imara Huweza Kutibu Hata Kansa:

Image may contain: one or more people, outdoor and closeup
Maradhi ya kansa yamekuwa yakiwasumbua watu wengi sana kwa nyakati za hivi karibuni. Hata hivyo kuna aina nyingi za kansa, mojawapo ni ile ya kibofu cha mkojo.
Kulingana na utafiti mmoja uliofanywa nchini marekani, imeonesha kwamba, msaada wa karibu unaotolewa na wanandoa kwa wanandoa wenzao ambao, wameathirika na ugonjwa wa kansa ya kibofu cha mkojo, ni aina mojawapo ya tiba inayoweza kuwafanya wagonjwa hao wajisikie vizuri na kuishi kwa muda mrefu.
Utafiti huo ulionyesha kwamba, watu wanaougua ugonjwa huo ambao wako kwenye ndoa, wana nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu zaidi ukilinganisha na wenzao ambao hawajaoa au kuolewa. Hali hii haichagui umri, rangi au hata kiwango cha athari ya ugonjwwa wenyewe.
Ndoa Imara Huweza Kutibu Hata Kansa.
Vilevile, tafiti mbalimbali za huko nyuma ziliwahi kuonesha kwamba, ndoa bora na imara zina uwezo wa kuwaongezea ahueni wanandoa wanaougua maradhi ya kansa
ya matiti na ile ya mkojo.
Watafiti hao walizidi kusema kwamba utafiti huo mpya unaweza ukawa na manufaa
zaidi kwa aina nyingine ya kansa. Hali kadhalika utafiti huo ulionesha
kwamba,wagonjwa wa kansa ambao walikuwa wamefiwa na wenzi wao wa ndoa na
wale waliotengana ama kutalikiana, waliathirika na ugonjwa huo zaidi.
Ingawa umri mkubwa nao ulichangia kwa kiwango kikubwa kwenye hali hiyo,
kutokuwa na mpenzi kulionesha wazi kuwa na madhara makubwa.
Sababu hasa, inayoyaofanya kuwa na tofauti hiyo, bado haijaulikani. Hata hivyo,
yapo maelezo machache yanayoweza kutolewa kuhusiana na hali hiyo. Kwa mfano,
mume au mke anaweza kumshauri mwenzi wake amwone mapema daktari, wakati
dalili za mwanzo kabisa za ugonjwa zinapojitokeza. Na pia anaweza kumshauri
mwenzake abadili mwenendo wa tabia zinazoweza kuuongeza madhara
yatokanayo na ugonjwa huu kwa mfano, kuacha kuvuta sigara, kwani tabia ya
uvutaji wa sifara huzidisha kiwango cha ugonjwa huu.
SOMA; Kama Hujui, Ndoa Imara Ni Tamu Kuliko Fedha.
Na pia msaada wa mume au mke, kwa njia moja au nyingine, huzipa nguvu
chembechembe hai za mwili zinazohusika na mfumo mzima wa wa ulinzi.
Uchunguzi huo ulionesha kuwa, wagonjwa wa kansa ya matiti waliokuwa
wameolewa na ambao walihisi kuwa wana uhusiano mzuri na imara na wenzi wao wa ndoa na kuwa wanapewa kila msaada wanaouhitaji, chembechembe zao hai zinazolinda mwili, zilionekana kufanya kazi kwa kiwango cha juu kabisa na hata
ziliweza kuua baadhi ya vijidudu vinavyosababisha ugonjwa huo.
Ndoa bora na imara imekuwa ikitajwa sana kama ni tiba inayoweza kutibu maradhi
mengi ikiwemo kansa na pia imekuwa ikielezwa kwamba, huufanya mwili wa
binadamu kuwa imara zaidi, watu wenye ndoa za mashaka na vurugu, wanapoingia
katika maradhi, wameonekana kudhoofu na pengine kufa haraka, ukilinganisha na
wale ambao wako kwenye ndoa imara.
Kwa hiyo hapa utajua, inaposisitizwa kwamba,wanandoa wajenge ukaribu ambao
utawezesha ndoa zao kuwa bora na imara, siyo tu kwa sababu ya ya kufurahia
mahaba, lakini pia ni kwa sababu ya kunusuru afya ya miili yao. Tafiti nyingi
zimekuwa zikionesha kwamba, wanandoa ambao wako kwenye vurugu za kindoa
hupata madhara mengi ya kimwili, wanawake wanaelezwa kwamba huathiriwa zaidi
na jambo hilo.
Kumbuka huu ni utafiti tu uliofanywa na wenzetu. Nikutakie siku njema na endelea
kujifunza kupitia Raha za chumbani kila siku, ili uweze kuboresha na kubadili maisha yako.
👇👇👇👇👇👇
#Follow Me😘
#Like My Page??
#ShareMy post😘
#Comment Below😘

Comments

Popular posts from this blog

UJUE MZUNGUKO WAKO WA HEDHI NA UFAHAMU SIKU ZA KUSHIKA MIMBA

Habari za leo rafiki yangu mpendwa, ni matumaini yangu unaendelea vizuri na kufurahia elimu uipatayo hapa pia napenda kuwapongeza wote wachukuao hatua kwa kutumia virutubisho vyetu na wale wanaouliza pale ambapo hawakupaelewa, hii ni kutokana na maoni yenu juu ya kuwafunza jinsi ya kuweza kuhesabu mzunguko wenu wa hedhi kupanga na kuepuka mimba, leo nipo hapa kuwajuza haya. Sasa basi kutokana na wanawake wengi kutokujua mizunguko yao ya hedhi, hivyo huwawia vigumu kujua ni siku gani iliyosahihi ili akutane na mumewe ama aepuke ili kubeba mimba au kutokushika mimba. Ni muhimu sana mwanamke kujua mzunguko wake wa hedhi, hii pia itakusaidia kujua siku hatari za kushika mimba na vile vile kukusaidia kuepuka mimba usiyoitarajia kwa kutumia kalenda yako kupanga tarehe yako.  NAMNA YA KUHESABU MZUNGUKO WAKO WA HEDHI Ili kujua siku nzuri ya kupata mimba au kuepuka ni lazima kwanza ujue siku ya KILELE BUKUKU (productive/fetal day) kwa maana kwamba ujue siku ambayo huitwa SIKU YA KUMI NA...

VYAKULA MUHIMU ZAIDI KWA MAMA MJAMZITO

LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NI MUHIMU SANA, KWANI LISHE HII HUTUMIKA KWA MAMA NA MTOTO ANAENDELEA KUKUA TUMBONI. KWA KAWAIDA MAHITAJI YA CHAKULA NA VIRUTUBISHO MWILINI MWA MWANAMKE HUONGEZEKA WAKATI WA UJAUZITO NA KADRI UJAUZITO UNAVYOENDELEA KUKUA, VIRUTUBISHO HIVYO HUTUMIKA KUJENGA MWILI WA MAMA NA MTOTO. HIVYO MAAMUZI YA LISHE AU LISHE MAMA ANAYOPATA HUATHIRI PIA MAENDELEO YA MTOTO ANAYEKUA MWILINI MWAKE. TUTAONA VYAKULA MUHIMU VYA KUZINGATIA LISHE BORA WAKATI WA UJAUZITO NA BAADHI YA VITU VYA KUKWEPA. Mama mjazito akipata mlo wenye mboga za majani Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini; Nafaka na Vyakula vya Wanga. Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi iki...

MKE MWEMA MTU HUPEWA NA BWANA. SIFA ZA MKE MWEMA

SIFA ZA MKE MWEMA 1) Kamwe usinyanyue sauti yako kwa mumeo kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara kuwa huna adabu na heshima. Pia niliwahi kufundisha hapa Ndoa Maridhawa kuwa radi haioteshi mazao yetu shambani licha ya kuwa na kelele na sauti kubwa, lakini mvua ambayo haina makelele huotesha mazao yetu shambani. 2) Usitangaze udhaifu wa mumeo kwa familia yako na marafiki zako. Linaweza kukuathiri wewe pia. Wewe ni mtunza siri wa mwenzako, na yeye ni mtunza siri wako. 3) Usitumie mihemko na hisia kali kuwasiliana na mumeo, hujui namna atakavyoitafsiri. Wanawake wenye mihemko iliyopitiliza hawawezi kuwa na ndoa yenye furaha. 4) Usimlinganishe mumeo na wanaume wengine, hujui undani wa maisha ya hao wengine. Ukiishambulia HADHI yake, upendo wake kwako utayeyuka. 5) Usiamiliane vibaya na marafiki wa mumeo kwa sababu tu huwapendi, mtu anayepaswa kuepukana nao ni mumeo. 6) Usisahay kuwa mumeo alikuoa wewe, hakumuoa huyo mfanyakazi wako wa ndani au mtu mwingine. Fany...