Maradhi ya kansa yamekuwa yakiwasumbua watu wengi sana kwa nyakati za hivi karibuni. Hata hivyo kuna aina nyingi za kansa, mojawapo ni ile ya kibofu cha mkojo. Kulingana na utafiti mmoja uliofanywa nchini marekani, imeonesha kwamba, msaada wa karibu unaotolewa na wanandoa kwa wanandoa wenzao ambao, wameathirika na ugonjwa wa kansa ya kibofu cha mkojo, ni aina mojawapo ya tiba inayoweza kuwafanya wagonjwa hao wajisikie vizuri na kuishi kwa muda mrefu. Utafiti huo ulionyesha kwamba, watu wanaougua ugonjwa huo ambao wako kwenye ndoa, wana nafasi kubwa ya kuishi muda mrefu zaidi ukilinganisha na wenzao ambao hawajaoa au kuolewa. Hali hii haichagui umri, rangi au hata kiwango cha athari ya ugonjwwa wenyewe. Ndoa Imara Huweza Kutibu Hata Kansa. Vilevile, tafiti mbalimbali za huko nyuma ziliwahi kuonesha kwamba, ndoa bora na imara zina uwezo wa kuwaongezea ahueni wanandoa wanaougua maradhi ya kansa ya matiti na ile ya mkojo. Watafiti hao walizidi kusema kwamba utafiti huo mpya unaweza ...